ANDIKO
LA KIMAHAKAMA [PETITION] KWA WANAFUNZI WOTE WENYE SIFA YA KUPIGA KURA WALIOKOSA
KUANDIKISWA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA KWA MFUMO MPYA WA BVR-BIOM
VOTERS REGISTRATION.
TANZANIA STUDENTS NETWORKING PROGRAMME (TSNP)
[MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA]
TSNP OFFICES AT SINZA DARAJAN-TP GROUND,
P.O.BOX 110024,
KINONDONI, DAR ES SALAAM TANZANIA.
Fb Page: Sauti Ya Wanafunzi Tanzania.
Contact: +255 765 443
728.
Simu kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa Taifa [NEC]
TSNP: Mzee shikamoo? Pole na majukumu.
Tulikuwa tunauliza suala la hatma ya wanafunzi wenye sifa ambao
hawajaandikishwa katika daftari la kudumu la kupiga kura kutokana na changamoto
tulizozieleza katika waraka wa Wanafunzi tuliouleta Tume ya Taifa ya uchaguzi
mnamo tar. 05/06/2015.
Mh. Jaji
Damian Lubuva: “Hapana
jana kwenye kikao cha waandishi wa habari na vyama vya siasa nilimake very clear
kwamba sasahivi hatuna jinsi Zaidi ya hapo. Suala la wanafunzi mnafanya
political na hatutakuwa na majibu Zaidi ya hayo tuliowapa nadhani ni juu yenu
kuamua what to do now?.
A.
Mtandao
Wa Wanafunzi Tanzania [TSNP-Tanzania Students Neyworking Programme.
Mtandao
wa wanafunzi Tanzania ni asasi ya kiraia isiyo ya kiserikali na haifungamani na
chama chochote iliyosajiliwa tarehe 23 Oktoba 2001[SO. NO. 42386]. Kuanzishwa
kwa mtandao huu kulitokana na kukosekana kwa umoja imara wa kutetea haki na
wajibu wa wanafunzi Tanzania.
Malengo ya Mtandao wa wanafunzi
Tanzania.
1. Kutetea
haki na wajibu wa wanafunzi nchini.
2. Kuanzisha
mtandao imara wa wanafunzi kutoka vyuo vikuu nchini.
3. Kushirikiana
na taasisi zingine kitaifa na kimataifa ambazo zinamalengo kama yetu.
Lengo la andiko la Kimahakama
[Petition].
Mtandao
Wa Wanafunzi Tanzania umeamua kuwa na mchakato wa kukusanya majina ya wanafunzi
wote nchini ambao wamekosa fursa ya kuandikishwa katika daftari la kudumu la
wapiga kura kutokana na changamoto ambazo tuliziainisha mbele ya Tume ya Uchaguzi
[NEC] bila kufanyiwa utatuzi na imekuwa ni utamaduni wa Tume ya Uchaguzi na
wizara ya Elimu kutoshirikiana ili wanafunzi washiriki bila vikwazo kuchagua
viongozi wao.
Hatua tulizozichukua kushughulikia
suala husika:
Ikumbukwe
tar. 29/05/2015 katika mkutano wa habari tulifafanua changamoto zinazowakumba
wanafunzi nchini kwa upande wa vyuo vikuu na shule za sekondari. Manamo tar.
05/06/2015 tulipata fursa ya kuwa na kikao na Mwenyekiti wa Tume ya taifa Mh.
Jaji Damian Lubuva ambapo alikiri changamoto tulizoziainisha katika waraka wa
wanafunzi na kuahidi kujibu waraka wetu mnamo tar.10/06/2015 baada ya kuonana
na sekretariet ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi {NEC].Mnamo tar. 10/06/2015 Tume ya
taifa ilijibu waraka wa wanafunzi ambapo sisi kama viongozi wa mtandao wa
Wanafunzi kwa niaba ya wanafunzi nchini hatukuridhika
na majibu ya tume dhidi ya waraka wetu kama viambatanishi vinavyojieleza. Nje
na kuwa na mawasiliano na Mh. Jaji Lubuva kwa simu tuliamua kuwa na mkutano na
waandishi wa habari tar. 11/07/2015 ili kuwataarifu wanafunzi nchi nzima majibu
ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na vile vile kutoa mapendekezo yetu ya mwisho kwa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC].
Changamoto tulizozianisha.
Kwa upande wa vyuo vikuu:
Historia
inatukumbusha kwamba, mwaka 2010 wanafunzi wa vyuo vikuu nchini walinyimwa
kupiga kura kwa sababu za makusudi ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC]
ilizifanya na huku wizara ya Elimu kutoa matangazo ya kufungua vyuo vikuu
nchini baada ya uchaguzi mkuu ili wanafunzi wasishiriki katika tukio la
Uchaguzi mkuu. Wanafunzi wa vyuo vikuu waliandikishwa katika daftari la kudumu
la kupiga kura wakiwa vyuoni na wakati wa Uchaguzi, vyuo vikuu vilikuwa
vimefungwa wengi wao wakiwa mikoani kitu ambacho kiliwanyima wanafunzi kupata
fursa na haki ya kuwachagua viongozi wao kwa sababu ya miongozo ya kupiga
kurainayotutaka kupiga kura katika kituo ulichoandikishiwa.
Kwa
tahadhari, mtandao wa wanafunzi Tanzania [TSNP] uliwajibika kuikumbusha Tume ya
Uchaguzi [NEC] historia husika na kuiomba Tume ya taifa kutatua changamoto
ambazo zilishaonekana hata kabla ya mchakato mpya wa BVR-Biometric Voters
Registration haswa kwa upande wa vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam.
Ikumbukwe
mchakato wa uandikishwaji wa watu katika mfumo mpya wa BVR ulitabiliwa kuanza
tar. 04/07/2014 ambapo vyuo vingi Dar es salaam vinakuwa vimefungwa na
wanafunzi wanakuwa wameenda mikoani ambako zoezi la BVR limemalizika. Tuliiomba
tume itoe muongozo wa namna ambavyo wanafunzi wenye sifa vyuo vikuu nchini
wataandikishwa ili kutokosa haki yao ya kuandikishwa. Tume ilijibu kwamba
itahakikisha watu wote wakiwemo wanafunzi wenye sifa wataandikishwa haswa
wakati wa mabadiliko ya taarifa kwa wapigakura watakaokuwa wamehama kuanzia
tar. 11-18/08/2015 kitu ambacho baada ya kumaliza zoezi Dar es salaam, tulimpigia
simu Mh. Jaji Lubuva kumuuliza suala la wanafunzi na majibu yalikuwa kama tulivyoyaainisha
ukurasa wa kwanza hapo juu.
Kwa upande wa Sekondari tuliiomba Tume ya Uchaguzi NEC itoe muongozo namna ambavyo wanafunzi walioenda JKT wataandikishwa, nmna ambavyo wanafunzi wa boding na wanafunzi wote nchini kwani ratiba za masomo zilikuwa zinaendelea huku mchakato wa BVR ukiendelea. Kwa taarifa zaidi ingia kwa blog yetu. www.wanafunzitz.blogspot.com
Mbaya
Zaidi hata kwa wale ambao waliandikishwa wakiwa vyuoni kunauwezekano mkubwa wa
kutopiga kura kwani Wizara ya Elimu imeshatoa matangazo kwamba vyuo vikuu
vitafunguliwa baada ya uchaguzi mkuu kumalizika hivyo wanafunzi walioandikishwa
wakiwa vyuoni hawatapata haki ya kupiga kura.
“Haki ya kupiga kura ni ya msingi
Zaidi kuliko haki ya kupigiwa kura”
Hitimisho
Letu.
Tumeadhimia kukusanya
majina ya wanafunzi wote nchini ambao wanasifa lakini wamekosa haki kuandikishwa
kwa sababu ya changamoto zilizojitokeza katika mchakato wa uandikishwaji ili
kuja kuiomba mahakama isirurhusu Uchaguzi Mkuu wa 2015 kufanyika mpaka pale
wanafunzi wenye sifa nchini wapate haki yao kuandikishwa ili washiriki katika
uchaguzi mkuu husika. Vile vile Mtandao huu unashirikiana na asasi zote za
kisheria na zisizo za kisheria ili kuhakikisha tunaungana katika kuhakikisha
wanafunzi wote wanapata haki yao ya kuandikishwa ili washiriki katika Uchaguzi
Mkuu wa 2015.
Na.
|
JINA
LA MWANAFUNZI
|
CHUO/SHULE
ANAYOSOMA
|
NAMBA
YA SIMU.
|
1
|
|
|
|
2
|
|
|
|
3
|
|
|
|
4
|
|
|
|
5
|
|
|
|
6
|
|
|
|
1.
|
|
|
|
2
|
|
|
|
3
|
|
|
|
4
|
|
|
|
5
|
|
|
|
6
|
|
|
|
7
|
|
|
|
8
|
|
|
|
9
|
|
|
|
10
|
|
|
|
11
|
|
|
|
12
|
|
|
|
13
|
|
|
|
14
|
|
|
|
15
|
|
|
|
16
|
|
|
|
17
|
|
|
|
18
|
|
|
|
19
|
|
|
|
20
|
|
|
|
21
|
|
|
|
22
|
|
|
|
23
|
|
|
|
………………………………………………. Imetolewa rasmi kuanzia tar. 18.08.2015