Sunday 2 August 2015

TSNP=WATAMBUE WANAFUNZI WALIOFUKUZWA UDSM MWAKA 2011 "HEROIC TRIPPLE ELLEVEN RIOT-11.11.2011.


MAHAKAMA YAWAACHIA HURU WANAFUNZI 51 WA UDSM
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewaachia huru wanafunzi 51 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) waliokuwa wakikabiliwa kwa pamoja na mashitaka ya kufanya mkusanyiko usio halali tarehe Novemba 11 mwaka 2011, eneo la Mlimani la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusababisha uvunjifu wa amani eneo la chuo hicho.

Wanafunzi hao waliachiwa jana na Hakimu Walialwande Lema aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo baada ya upande wa mashitaka ulioongozwa na Wakili wa Serikali, Ladslaus  Komanya kushindwa kuleta mashahidi mahakamani huku wakitoa sababu mbalimbali. Komanya alidai kuwa  washtakiwa hao wakiwa kwenye mkusanyiko huo haramu kwa lengo la kufanya mgomo, askari wa Jeshi la Polisi waliwataka watawanyike, lakini hata hivyo wanafunzi hao walikaidi amri hiyo na kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Hata hivyo washitakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, walikana mashtaka hayo na waliachiwa huru baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika ambaye alisaini bondi ya Shilingi milioni moja.

Baada ya kuachwa huru, wanafunzi hao waliondoka mahakamani hapo kwa furaha huku wakikumbatiana na wengine wakisali.

Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Lema alisema kuwa anatupilia mbali maombi ya upande wa mashitaka yaliyokuwa yakiomba ahirisho la kesi hiyo kwa mara nyingine wakidai kuwa mashahidi wao ambao ni askari wako katika Sensa ya Watu na Makazi.

Lema alisema kuwa sensa ni muhimu kama ilivyo kesi hiyo, lakini maombi yao hayakufuata taratibu za sheria ambapo kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 225 (4) Sheria ya  Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA), sura ya 20 kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kuliendesha shtaka hilo.

“Agosti 13 mwaka huu kulikuwa na ahirisho ambapo sababu ilikuwa hakuna mashahidi kwa sababu wako katika mgomo wa madaktari, leo tena mnaleta sababu kuwa wako katika sensa inaonesha mmedharau amri ya Mahakama,” alisema Hakimu.

Alisema amri ya mwisho aliyoitoa ilikuwa ahirisho la Agosti 13 mwaka huu hivyo upande wa mashitaka umedharau amri ya Mahakama na kwa maana hiyo anawaachia huru washitakiwa wote chini ya kifungu cha sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai kifungu cha 225 (5) sura ya 20.

Awali wakili wa upande wa mashitaka, Prosper Mwangamila alidai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa akaomba iahirishwe hadi Jumatatu. Wakili wa washitakiwa hao, Reginard Martin akijibu hoja hiyo aliiomba Mahakama kutokubali ombi hilo na badala yake kesi ifutwe washitakiwa waachiwe huru.

Baadhi ya majina ya wanafunzi walioachwa huru ni Mwambapa Elias, Evarist Ambrose, Baraka Monas, Hellen Moshi, Alphonce Lusako, Matrona Babu, Rolanda Wilfred, Godfrey Deogratius, Moris Denis and Evon Gumbi.Others are Lugiko Mathias, Ndimbo Jabir, Evarist Wilson, Cornel Rwaga Mushi, Mlazi Kumbuka, Rehema Munuo, Glory Masawe, Happy Amulike, Elias Mpangala, Frida Timothy, Stella Mofe, Betwel Martin, Mmasi Stephen na Lugemalila Venance na wengineo.
---

No comments:

Post a Comment

Students!!!!!!!!!
For Nation....

Students!!!!!!!!!
Together we have the power.