Friday 31 July 2015

TSNP & AZAM TV LIVE 30.07.2015. CHANGAMOTO ZIWAKUMBAZO WANAFUNZI NCHINI KATIKA MCHAKATO WA BVR.

Ndugu Alphonce Lusako akiwa Katibu wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania akiwa anahojiwa na Mtangazaji wa Azam TV

HAYA NI MAPENDEKEZO YETU YA MWISHO KWA TUME YA UCHAGUZI YA TAIFA JUU YA CHANGAMOTO ZIWAKUMBAZO WANAFUNZI NCHINI. NA HII NDIO PRESS RELEASE YA MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA TULIOITOA JANA KWA VYOMBO VYA HABARI. MAADHIMIO YA MTANDAO WA WANAFUNZI NCHINI {TSNP} DHIDI YA MAJIBU YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI {NEC} JUU YA CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA WANAFUNZI KATIKA MCHAKATO WA UANDIKISHWAJI WA MFUMO MPYA WA BVR-BIOMETRIC VOTER REGISTRATION.


Ndugu wahandishi wa habari, ikumbukwe kwamba tarehe 29/05/2015 mtandao wa wanafunzi {TSNP} ulitoa tamko lililoitaka Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) ieleze namna ambavyo wanafunzi wa vyuo vikuu na wale wa shule za sekondari nchini watakavyooandikishwa ilihali wanakabiriwa na changamoto mbalimbali mathalani suala la wanafunzi walioenda JKT, Wanafunzi wa sekondari ambao wanaendelea na ratiba ya masomo huku mchakato wa uandikiswaji ukiendelea, suala la uchaguzi mkuu kufanyika wakati shule za sekondari zikiendelea na ratiba za masomo na suala la wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wapo Dar es salaama na Mchakato wa uandikishwaji unaanza wakati vyuo vingi vimefungwa na wanavyuo wanarudi mikoani ambako mchakato wa uandikishwaji ushafanyika. Pamoja na changamoto hizo ambazo mtandao wa wanafunzi Tanzania tulizieleza.


 Tarehe 05/7/2015 wawakilishi wa wanafunzi wa vyuo vikuu walienda kuonana na mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi Jaji Damian Lubuva kumueleza changamoto husika. Lakini tarehe 10/07/2015 Tume ya taifa ya uchaguzi kupitia kwa kaimu mkurugenzi wa uchaguzi Dr. Sisti Cariah ilitoa waraka wa kujibu wawakilishi wa wanafunzi wa vyuo vikuu waliokutana na mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi. Tunasikitika na ukweli kwamba, majibu ya tume hayakujibu haja na matarajio ya wanafunzi wa vyuo vikuu na shule za sekondari kwa ujumla wake na kuwafanya wanafunzi wengi nchini kuwa na sintofahamu juu ya hatima yao ya kuanddikishwa katika mfumo mpya wa BVR ili kupata haki yao ya kuchagua viongozi wao.


Mapendekezo:


Tunapenda kusema kwamba, Mtandao wa Wanafunzi Tanzania haujaridhishwa kabisa na majibu ya tume na unatoa mapendekezo ya mwisho kwa Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) yatakayowawezesha wanafunzi wenye sifa nchini waliokosa kujiandikisha kwa sababu ya changamoto tulizozieleza hapo juu waweze kujiandikisha. Mosi, Wakati wa uhamishwaji wa taarifa za wapiga kura {kati ya 11-18 agust 2015} ,tunaiomba tume ipeleke BVR Kits katika kila halmashauri ya nchi hii ili kuhakikisha wananchi wenye sifa wakiwemo wanafunzi ambao hawajaandikishwa waandikishwe


Pili, Mtandao wa Wanafunzi unaitaka Tume ya taifa ya uchaguzi iweze kupeleka mashine za BVR kit vyuoni kwa vyuo vyote vya Dar es salaam ambavyo vitakuwa bado havijafungwa wakati zoezi la uandikishaji litakapokuwa likiendelea mkoani Dar es salaam.


Tatu, Mtandao wa wanafunzi Tanzania unapenda kusisitiza tena Tume ya taifa ya uchaguzi kwamba, endapo wanafunzi wataikosa haki yao hii ya kikatiba ya kujiandikisha na kupiga kura basi wanafunzi wote kwa umoja wetu pamoja na hatua nyingine tutakazo zichukua tutapinga kufanyika kwa uchaguzi mkuu 25 oktober 2015 mahakamani mpaka pale tutapoona wanafunzi wote wenye sifa wataandikishwa.


Tunaiomba Tume ya Taifa ya Uchaguziishirikiane na wizara ya Elimu ili wakati wa uchaguzi Shule za sekondari zifungwe ili wanafunzi wote wenye sifa washiriki kuchagua viongozi wao.


Hitimisho:


Kwa tahadhari, Sisi kama mtandao wa wanafunzi Tanzania tunafahamu mambo yaliyotokea mwaka 2009 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, danganya toto zile zile ndizo zinaendelea wakati huu, Inachokifanya Tume ya Taifa ya Uchaguzi {NEC} ni kuairisha tatizo. Mwaka 2015 hatutakubali kudanganywa na tupo tayari kupambana kwa mujibu wa sharia za nchi hii ili kuhakikisha tunapata haki zetu. Vile vile tunawaomba wanavyuo wote nchini kwa gharama yoyote ile wafike Dar es Salaam kwa ajili ya kuandikishwa pale zoezi litapoanza {16 Julai 2015}.


By TSNP General Secretary
Alphonce Lusako M.
tsnp.students@yahoo.com

No comments:

Post a Comment

Students!!!!!!!!!
For Nation....

Students!!!!!!!!!
Together we have the power.