Saturday 1 August 2015

TSNP & SAHARA SOLIDARITY COMMITTEE IN TANZANIA. 25.07.2015


Comrade ADO SHAIBU among of the initiator of the idea in left side waiting to be welcomed for speech.
Comrade Mason Kimbo. TSNP International affairs asking question to hight table concerning kind of rights which citizen of West sahara are lacking
Comrade Alphonce Lusako M. TSNP general secretary congratulating small committee who initiate the idea and promising them to link their idea with Tanzania students all over the country. he used to trace back the back ground of his NGO [TSNP] in 1960,s when there were national movement of students against Unilateral declaration of southern Rhodesia independence and he promised to cooperate with the launched committee to voice west Saharan people rights
On the right side of the image is comrade Gwakisa Mtachaula a member of TSNP
TSNP international affairs comrade Mason Kimbo in group photo





MWALIKO WA TSNP KUTOKA KWA KAMATI NDOGO YA UMOJA WA SAHARA NCHIN
I TANZANIA.


Sisi vijana wa Kitanzania, baada ya kutafiti, kutafakari na kujadili, tumekusudia kuunda Umoja wa Mshikamano baina ya Watu wa Sahara Magharibi na Tanzania. Lengo hasa la Kamati husika ni kuziendeleza jitihada za miaka mingi za Tanzania katika kuzisaidia nchi za Kiafrika katika Kujikomboa kutoka katika ukoloni na, kama ilivyo kwenye suala la Sahara Magharibi, kukaliwa kimabavu na Moroko. Siku ya Jumamosi (Tarehe 25/7/2015) tutafanya uzinduzi wa kamati (Tanzania-Saharawi Solidarity Committee-TASSC). Watu wote mnakaribishwa kwenye tukio hili litalofanyika katika Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini (Mkabala na Shule ya Jitegemee, Dar) kuanzia saa tano kamili asubuhi hadi saa saba kamili mchana. Mgeni wa heshma atakuwa Balozi wa Sahara Magharibi nchini. Itahudhuriwa pia na Balozi wa Algeria. MADA: Historia ya Suala la Sahara Magharibi-Balozi, Sahara Magharibi Malengo ya Kamati na Mchango wa Tanzania Katika Ukombozi wa Afrika- Ado Shaibu Suala la Sahara Magharibi katika Muktadha wa Ukombozi wa Afrika-Alfayo Ngogo MUZIKI: Maembe Vitali Hii pia ni fursa kwetu vijana, wake kwa waume, kukutana, kufahamiana zaidi, kubadilishana mawazo na kujadili. Mimi nitakuwepo. Bila shaka nawe utakuwepo. Karibuni tufufue, Zama zilizopotea, Karibuni tuzindue, La ukombozi Jukwaa. Thibitisha ushiriki wako kwa Ado Shaibu (0653619906) Uanzishwaji wa kuunda kamati ya vuguvugu la Watu wa Saharawi ni jambo jema kwa muktadha wa ukombozi wa Afrika isiyo na chembe ya ukandamizaji dhidi ya mataifa madogo.ilikuwa tarehe 25/07 vijana mbalimbali walikusanyika kupaza sauti juu ya ukandamizaji wa Morroco dhidi ya Sahara Magharibi

No comments:

Post a Comment

Students!!!!!!!!!
For Nation....

Students!!!!!!!!!
Together we have the power.