Thursday 20 August 2015

ANDIKO LA KIMAHAKAMA LA MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA [TSNP] LILILOTOLEWA RASMI TAR. 18.08.2015 KWA WANAFUNZI WOTE NCHINI AMBAO HAWAJAPATA FURSA YA KUANDIKISHWA ILI HALI WANASIFA YA KUANDIKISHWA.




ANDIKO LA KIMAHAKAMA [PETITION] KWA WANAFUNZI WOTE WENYE SIFA YA KUPIGA KURA WALIOKOSA KUANDIKISWA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA KWA MFUMO MPYA WA BVR-BIOM VOTERS REGISTRATION.
TANZANIA STUDENTS NETWORKING PROGRAMME (TSNP)
[MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA]
TSNP OFFICES AT SINZA DARAJAN-TP GROUND,
P.O.BOX 110024,
KINONDONI, DAR ES SALAAM TANZANIA.
Fb Page: Sauti Ya Wanafunzi Tanzania.
Contact:      +255 765 443 728.

Simu kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa Taifa [NEC]
TSNP: Mzee shikamoo? Pole na majukumu. Tulikuwa tunauliza suala la hatma ya wanafunzi wenye sifa ambao hawajaandikishwa katika daftari la kudumu la kupiga kura kutokana na changamoto tulizozieleza katika waraka wa Wanafunzi tuliouleta Tume ya Taifa ya uchaguzi mnamo tar. 05/06/2015.

Mh. Jaji Damian Lubuva: “Hapana jana kwenye kikao cha waandishi wa habari na vyama vya siasa nilimake very clear kwamba sasahivi hatuna jinsi Zaidi ya hapo. Suala la wanafunzi mnafanya political na hatutakuwa na majibu Zaidi ya hayo tuliowapa nadhani ni juu yenu kuamua what to do now?.

A.    Mtandao Wa Wanafunzi Tanzania [TSNP-Tanzania Students Neyworking Programme.

Mtandao wa wanafunzi Tanzania ni asasi ya kiraia isiyo ya kiserikali na haifungamani na chama chochote iliyosajiliwa tarehe 23 Oktoba 2001[SO. NO. 42386]. Kuanzishwa kwa mtandao huu kulitokana na kukosekana kwa umoja imara wa kutetea haki na wajibu wa wanafunzi Tanzania.

Malengo ya Mtandao wa wanafunzi Tanzania.
1.      Kutetea haki na wajibu wa wanafunzi nchini.
2.      Kuanzisha mtandao imara wa wanafunzi kutoka vyuo vikuu nchini.
3.      Kushirikiana na taasisi zingine kitaifa na kimataifa ambazo zinamalengo kama yetu.

Lengo la andiko la Kimahakama [Petition].
Mtandao Wa Wanafunzi Tanzania umeamua kuwa na mchakato wa kukusanya majina ya wanafunzi wote nchini ambao wamekosa fursa ya kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kutokana na changamoto ambazo tuliziainisha mbele ya Tume ya Uchaguzi [NEC] bila kufanyiwa utatuzi na imekuwa ni utamaduni wa Tume ya Uchaguzi na wizara ya Elimu kutoshirikiana ili wanafunzi washiriki bila vikwazo kuchagua viongozi wao.

Hatua tulizozichukua kushughulikia suala husika:
Ikumbukwe tar. 29/05/2015 katika mkutano wa habari tulifafanua changamoto zinazowakumba wanafunzi nchini kwa upande wa vyuo vikuu na shule za sekondari. Manamo tar. 05/06/2015 tulipata fursa ya kuwa na kikao na Mwenyekiti wa Tume ya taifa Mh. Jaji Damian Lubuva ambapo alikiri changamoto tulizoziainisha katika waraka wa wanafunzi na kuahidi kujibu waraka wetu mnamo tar.10/06/2015 baada ya kuonana na sekretariet ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi {NEC].Mnamo tar. 10/06/2015 Tume ya taifa ilijibu waraka wa wanafunzi ambapo sisi kama viongozi wa mtandao wa Wanafunzi kwa niaba ya wanafunzi  nchini hatukuridhika na majibu ya tume dhidi ya waraka wetu kama viambatanishi vinavyojieleza. Nje na kuwa na mawasiliano na Mh. Jaji Lubuva kwa simu tuliamua kuwa na mkutano na waandishi wa habari tar. 11/07/2015 ili kuwataarifu wanafunzi nchi nzima majibu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na vile vile kutoa mapendekezo yetu ya mwisho kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC].

Changamoto tulizozianisha.

Kwa upande wa vyuo vikuu:

Historia inatukumbusha kwamba, mwaka 2010 wanafunzi wa vyuo vikuu nchini walinyimwa kupiga kura kwa sababu za makusudi ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC] ilizifanya na huku wizara ya Elimu kutoa matangazo ya kufungua vyuo vikuu nchini baada ya uchaguzi mkuu ili wanafunzi wasishiriki katika tukio la Uchaguzi mkuu. Wanafunzi wa vyuo vikuu waliandikishwa katika daftari la kudumu la kupiga kura wakiwa vyuoni na wakati wa Uchaguzi, vyuo vikuu vilikuwa vimefungwa wengi wao wakiwa mikoani kitu ambacho kiliwanyima wanafunzi kupata fursa na haki ya kuwachagua viongozi wao kwa sababu ya miongozo ya kupiga kurainayotutaka kupiga kura katika kituo ulichoandikishiwa.
Kwa tahadhari, mtandao wa wanafunzi Tanzania [TSNP] uliwajibika kuikumbusha Tume ya Uchaguzi [NEC] historia husika na kuiomba Tume ya taifa kutatua changamoto ambazo zilishaonekana hata kabla ya mchakato mpya wa BVR-Biometric Voters Registration haswa kwa upande wa vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam.

Ikumbukwe mchakato wa uandikishwaji wa watu katika mfumo mpya wa BVR ulitabiliwa kuanza tar. 04/07/2014 ambapo vyuo vingi Dar es salaam vinakuwa vimefungwa na wanafunzi wanakuwa wameenda mikoani ambako zoezi la BVR limemalizika. Tuliiomba tume itoe muongozo wa namna ambavyo wanafunzi wenye sifa vyuo vikuu nchini wataandikishwa ili kutokosa haki yao ya kuandikishwa. Tume ilijibu kwamba itahakikisha watu wote wakiwemo wanafunzi wenye sifa wataandikishwa haswa wakati wa mabadiliko ya taarifa kwa wapigakura watakaokuwa wamehama kuanzia tar. 11-18/08/2015 kitu ambacho baada ya kumaliza zoezi Dar es salaam, tulimpigia simu Mh. Jaji Lubuva kumuuliza suala la wanafunzi na majibu yalikuwa kama tulivyoyaainisha ukurasa wa kwanza hapo juu. 

Kwa upande wa Sekondari tuliiomba Tume ya Uchaguzi NEC itoe muongozo namna ambavyo wanafunzi walioenda JKT wataandikishwa, nmna ambavyo wanafunzi wa boding na wanafunzi wote nchini kwani ratiba  za masomo zilikuwa zinaendelea huku mchakato wa BVR ukiendelea. Kwa taarifa zaidi ingia kwa blog yetu. www.wanafunzitz.blogspot.com

Mbaya Zaidi hata kwa wale ambao waliandikishwa wakiwa vyuoni kunauwezekano mkubwa wa kutopiga kura kwani Wizara ya Elimu imeshatoa matangazo kwamba vyuo vikuu vitafunguliwa baada ya uchaguzi mkuu kumalizika hivyo wanafunzi walioandikishwa wakiwa vyuoni hawatapata haki ya kupiga kura.
“Haki ya kupiga kura ni ya msingi Zaidi kuliko haki ya kupigiwa kura”
Hitimisho Letu.
Tumeadhimia kukusanya majina ya wanafunzi wote nchini ambao wanasifa lakini wamekosa haki kuandikishwa kwa sababu ya changamoto zilizojitokeza katika mchakato wa uandikishwaji ili kuja kuiomba mahakama isirurhusu Uchaguzi Mkuu wa 2015 kufanyika mpaka pale wanafunzi wenye sifa nchini wapate haki yao kuandikishwa ili washiriki katika uchaguzi mkuu husika. Vile vile Mtandao huu unashirikiana na asasi zote za kisheria na zisizo za kisheria ili kuhakikisha tunaungana katika kuhakikisha wanafunzi wote wanapata haki yao ya kuandikishwa ili washiriki katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Na.
JINA LA MWANAFUNZI
CHUO/SHULE ANAYOSOMA
NAMBA YA SIMU.
1



2



3



4



5



6



1.



2



3



4



5



6



7



8



9



10



11



12



13



14



15



16



17



18



19



20



21



22



23




……………………………………………….                        Imetolewa rasmi kuanzia tar. 18.08.2015
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania [TSNP]